historia

Hospitali ya Mkoa Geita ilipandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa tarehe 01/07/2016, awali ilikuwa hospitali ya wilaya Geita ambayo ilianzishwa mwaka 1956 na kufunguliwa rasmi mwaka 1958 ikitoa huduma kwa wakazi wa jimbo la Geita (Geita Province) lililojumuisha halmashauri za Geita na Sengerema kabla ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 pamoja na wakazi wa baadhi ya maeneo ya Chato na Biharamulo.

Hospitali ya Mkoa baada ya kupandishwa hadhi inahudumia wakazi wapatao 1,949,694 kutoka Halmashauri za Mji wa Geita, Nyang’hwale, Bukombe, Mbogwe Pamoja na wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato na Halmashauri ya Wilaya Geita.